Maneno ya Ukaribisho toka kwa Baba Paroko

Kwa niaba ya waamini wa Parokia ya Mtakatifu Maria De Mattias – Mivumoni, Niwakaribishe kutembelea tovuti yetu. Parokia ya Mtakatifu Maria De Mattias - Mivumoni, ipo katika JImbo Kuu la Dar es Salaam katika Dekania ya Mtakatifu Gaspari Del Bufallo na kuwa mojawapo ya Parokia 17 anzilishi zinazounda Jimbo jipya la Bagamoyo. Parokia ipo eneo la Mivumoni, kata ya Wazo. Parokia hii inaadhimisha ibada zote kwa kufuata litrijua na miongozo yote ya Kanisa Katoliki. Tunawakiribisha waamini wote na wenye mapenzi mema kufika na kuja kusali pamoja nasi na kushiriki kwa pamoja katika kutakatifuza maisha yetu. Mwenyezi Mungu, anatupenda tuwe na upendo na tuweze kupendana kati yetu, kwa kushirikishana Ufalme wa Mungu na kufanya maisha ya hapa duniani kuwa ya upendo na amani. Kutokana na mabadiliko haya ya kuundwa kwa Jimbo jipya la Bagamoyo, Baba Askofu Mhashamu Stefano Lameck Musomba, OSA. Askofu wa Jimbo la Bagamoyo aliunda Dekania mpya 5 za Jimbo la Bagamoyo, na kutangaza viongozi. DEKANIA TANO ZA JIMBO KATOLIKI BAGAMOYO, 1. DEKANIA YA TEGETA, Parokia ya Tegeta, Parokia ya Boko, Parokia ya Bahari Beach, Parokia ya Ununio, Parokia ya Mbweni Teta, Parokia ya Tegeta Kibaoni na Parokia Teule ya Mbweni JKT, Dekano ni Fr. Emmanuel Makusaro. 2. DEKANIA YA MIVUMONI, Parokia ya Mivumoni, Parokia ya Wazo Hill, Parokia ya Madale, Parokia ya Mbopo, Parokia ya Nyakasangwe, Parokia ya Muungano, Dekano ni Fr. Joseph Lwena. 3. DEKANIA YA BUNJU, Parokia ya Bunju, Parokia ya Mbweni Mt. Raphael, Parokia ya Mbweni Mpiji, Parokia ya Kiharaka, Parokia ya Kerege, Parokia ya Kinondo, Parokia Teule ya Zinga, Dekano ni Fr. Edwin Deno. 4. DEKANIA YA BAGAMOYO, Parokia ya Moyo Safi wa Bikira Maria, Parokia Epifania, Parokia ya Kiwangwa, Parokia ya Mandela, Parokia ya Lugoba, Parokia Teule ya Makurunge. Dekano ni Fr. Elias Petro. 5. DEKANIA YA CHALINZE, Parokia ya Chalinze, Parokia ya Mdaula, Parokia ya Ngerengere, Parokia ya Bwawani, Dekano ni Fr. Patrick Bung'alo.
Fr. Francis Pastory Malele.