PADRE DOMINIK MAVULA C.PP.S NA TAFAKARI YA IBADA YA MOYO SAFI NA JUMAMOSI YA KWANZA KWA HESHIMA YA BIKIRA MARIA
Ibada kwa Moyo safi wa Maria ilianzishwa rasmi na Mt.Yohane Eudes (1601-1670) huyu aliitwa Baba wa Ibada hii. Aliiweka ibada hii jumamosi ya kwanza baada ya Sherehe ya Moyo Mt. wa Yesu. Maria Inglese alikuja tena kufunuliwa ibada hii mwaka 1889 na Mama Maria mwenyewe. Ndiye aliyeambiwa juu ya jumamosi 5 za kwanza mfululizo kutolea kwa Moyo safi wa B. Maria. Binti huyu ndiye aliyetunga mfululizo wa sala msingi za ibada hii katika maelekeo ya toba. Baba Mt. Pio X alipitisha rasmi sala hizi. Mama Maria akaja kukazia Ibada hii katika matokeo ya hadharani (public apparition)ya Fatima na matokeo ya ndani (private apparition) ya Lucia peke yake. Kumbe heshima kwa Jumamosi ya kwanza ya mwezi ni agizo toka Mbinguni kwa ajili ya dhambi zetu na za Dunia nzima. Tuungame, tupokee Ekaristi, tusali Rosari na tutafakari walau kwa Robo saa kila Jumamosi ya kwanza ya mwezi.